Mieko Nagaoka: Mjapan Mwenye Miaka 100 Aliyeweka Rekodi ya Dunia ya Kuogelea
by on August 28, 2015 in News

mieko-nagaoka

Nikiwa kwenye gari langu katika mizunguko yangu Jijini Los Angeles; kama kawaida yangu niliperuzi radio za Tanzania katika TuneIn, nikatua Tbc Fm nikakutana na wimbo wangu dundika ukichezwa. Nikasema ngoja nisikilize mpaka mwisho wa kipindi; Mara kikafuata kipindi cha radio Japan wakawa wanamzungumzia (marudio) huyu bibi Mjapani wa miaka mia moja jinsi alivyoanza kujifunza kuogelea akiwa na umri wa miaka 80. Nikavutiwa nikahamasika nikajisemea moyoni kweli duniani hamna kinachoshindikana kufanyika katika umri wowote ule. Mtu anaweza kufanya chochote kizuri kuanzia umri mdogo hadi miaka 100 na zaidi, ilimradi kusiwe na visingizio. Mieko Nagaoka alianza kujifunza kuogelea akiwa na umri wa miaka 80. Sasa akiwa na miaka 100 ameshaweka rekodi ya dunia ya kuogelea na kushinda 25m. Na hana mpango wa kustaaafu. Anatarajia kuendelea kuogelea mpaka pale mwenyezi mungu atakapomruhusu kuishi.

Amenivutia na kunitia moyo na kunipa nguvu zaidi ya kufanya kazi ninazozipenda kwa bidii hata nikikutana na ukuta nisikate tamaa na kutoruhusu visingizio kutawala maisha yangu.

Nimezungukwa na watu wa umri mbalimbali, wengi wao kwa upeo wamngu ambo naona kwanza ndo maisha yanaanza; utasikia ,oh nimezeeka kitu fulani siwezi fanya, hivyo naachia watoto. Ukiangalia ana miaka 30.

Wenye miaka 50, 60 na 70 utasikia duh nguvu zimeniishia mambo mengine nawaachia watoto wafanye, sasa kama mtu mwenye umri huu asha kata tamaa ya maisha, mwenye 100 ambaye bado anahamaki ya kuendelea kuvunja rekodi ya dunia asemeje?

Natoa changamoto kwa yeyote yule anayejiona ni mzee hawezi kufanya kitu chochote kile kwamba umri umeenda. Kama we ndo una umri kati ya 50 na 90 ndo kwanza kumekucha. Usilale. Anza kufanya kitu unachokipenda sasa hivi hujachelewa. Umri si tija ni namba tu. Hata Nelson Mandela alikuwa rais wa Africa kusini baada yakutoka jela akiwa na umri wa miaka 75.

Natumaini huu ujumbe utakupa hamaki na hamasa kama ulivyonipa mimi.

Leave a Reply

© Erica Lulakwa, 2015